Viongozi wa nchi za Afrika Magharibi
wamempa Yahya Jammeh fursa ya mwisho kuachia madaraka, huku wanajeshi
wa Senegal wakiingia nchini Gambia.
Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi (Ecowas) inaunga mkono Adama Barrow, ambaye aliapishwa kuwa rais mpya wa Gambia katika ubalozi wa nchini hiyo nchini Senegal.
Mwenyekiti wa tume ya Ecowas, Marcel Alain de Souza, alisema iwapo mkutano huo utakaoongozwa na Bw Conde hautafaulu, basi hatua ya kijeshi itafuata.
"Iwapo kufikia saa sita mchana, yeye (Bw Jammeh) hatakubali kuondoka Gambia chini ya Rais Conde, tutaingilia kijeshi," amesema.
Wanajeshi wa Ecowas walisema hawakukumbana na pingamizi zozote kutoka kwa wanajeshi wa Gambia walipoingia nchini humo Alhamisi baada ya kuapishwa kwa Barrow.

Wanajeshi kutoka Senegal na nchi nyingine za Afrika Magharibi waliingia Gambia baada ya makataa mengine aliyopewa Bw Jammeh kuondoka kumalizika.
Bw Jammeh, ambaye bado yupo nchini Senegal amesema hatarejea mji mkuu wa Gambia, Banjul, hadi operesheni ya kijeshi imalizike.
Hatua ya Ecowas kutaka kumtoa kwa nguvu Jammeh inaungwa mkono na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lenye wanachama 15, ingawa baraza hilo lilisisitiza kwamba suluhu ya amani inafaa kupoewa kipaumbele.
0 maoni:
Chapisha Maoni