Pages

Alhamisi, 23 Februari 2017

ALIKIBA NA YVONE CHAKACHAKA NDANI YA STUDIO MOJA KUFANYA REKODI

Alikiba bado anaendelea kufanya vizuri katika muziki wake na sasaivi anatamba na video ya Aje aliyoifanyia remix ambayo inafanya vizuri katika mtandao wa you tube ikiwa  tayari imeshaangaliwa na watazamaji idadi zaidi ya laki tatu (3). Kwa sasa anawaandaa mashabiki wake kupokea wimbo mzuri aliomshirikisha msanii kutoa nje ya Tanzania.
Image result for ali kiba
Alikiba sasa yupo mbioni kutoa ngoma yake kali ambayo amemshirikisha msanii kutoka South Afrika msanii mkongwe sana ambaye kwa miaka ya nyuma nyimbo  zake zilipendwa na watu wengi, alitamba na nyimbo yake ya Umqumbothi (African beer), anajulikana kwa jina la Yvone Chakachaka.
Image result for yvonne chaka chaka
Jana usiku Alikiba kupitia ukurasa wake  wa instagram alirusha mtandaoni baadhi ya picha zake akiwa na Yvone Chakachaka zikionesha anatengeneza ngoma na msanii huyo mkongwe, moja ya picha ilibeba maneno haya.
”Jana usiku rekodi ya mwisho na Mama @Yvonne Chakachaka. Ninashukuru na kweli nina furaha juu ya mradi wetu. Asante sana mama kwa kila kitu”.
Pia yvone Chakachaka kupitia kurasa wake wa twitter ametweet, ”Jana mimi na mwanangu tumemaliza kurekodi’.

0 maoni:

Chapisha Maoni