Na Alexx Mwenda
Huu ndio ushahidi wa Diamond Platnumz kununua watazamaji ‘Youtube’.
Huwezi kutaja wasanii ambao wamechangia kupeperusha bendera ya muziki
wa kizazi kipya duniani bila kutaja jina la Nassib Abdul maarufu kama
Diamond Platnumz
Hoja za kununua watazamaji katika mtandao wa Youtube zilichukua
nafasi miezi kadhaa nyuma kati ya Ommy Dimpoz na Diamond Platnumz. Hoja
zao zilifika mbali hata kupelekea kutoleana kauli zisizofaa mbele ya
mashabiki kupitia mitandao ya kijamii na media kwa ujumla.
Lakini pia mashabiki na wasanii wanapaswa kujua kuwa hakuna jambo
baya kununua watazamaji katika mtandao wa Youtube, ni katika hali ya
kujitangaza zaidi kwa kutumia fursa ya mtandao. Jambo baya ni kudangaya
kuwa watazamaji hao msanii anawapata kwa hali ya kawaida sio ya kununua
kwa maana ya “Kupromote”
Wimbo huo umekuwa ‘Promoted’ kwenye mtandao wa Youtube kama tangazo ili uweze kupata watazamaji wengi kwa wakati mfupi. Hivyo unapoingia tu katika mtandao wa Youtube ni lazima ukutane na wimbo huo.
Tazama hapa chini ushahidi huu.

0 maoni:
Chapisha Maoni