Na Alex Mwenda
Mshambuliaji wa zamani wa klabu za Yanga na Simba, Emmanuel Okwi leo
ameanza rasmi kuitumikia klabu yake ya SC Villa Jogoo kwa kuichezea
mechi ya kwanza dhidi ya Bright Stars.
Okwi alianza mechi hio ya Ligi Kuu nchini Uganda iliyomalizika kwa
sare ya bila kufungana na kuwaacha Villa wakiwa nyuma ya vinara KCCA kwa
pointi tatu.
Awali Okwi aliuambia mtandao huu kuwa yupo fiti kucheza mchezo wa leo lakini hafahamu kama kocha atamuanzisha.
Wageni Villa walitawala mchezo huo kwa kiasi kikubwa lakini Okwi na
wenzake walishindwa kabisa kuisumbua safu ya ulinzi ya Bright Stars.
Okwi amejiunga na Villa kwa mkataba wa miezi sita akitokea klabu ya
Denmark aliyoamua kuachana nayo baada ya kukosa namba katika kikosi cha
kwanza kwa muda mrefu.
0 maoni:
Chapisha Maoni