Chuo kikuu cha Lagos nchini Nigeria kimepiga marufuku wanafunzi kuvaa nguo zinazobana mwili.
Taarifa
iliyotolewa kwa wanafunzi chuoni hapo inasema wanapaswa kuonekana
nadhifu wawapo katika maeneo ya chuo, na kwamba uvaaji wa nguo za kubana
ama zinazoonesha miili yao, sio jambo la kufaa.
Chuo kimepiga
marufuku nguo zote ambazo zinaonesha maeneo nyeti ya sehemu za mwili
kama vile kifua, tumbo, sehemu ya matiti, makalio.
Raia wengi wa
Nigeria wamekuwa wakipendelea kuvaa nguo zenye staha, lakini katika
kizazi cha vijana wa sasa mara mara nyingi wamekuwa wakidharau maadili
ya mavazi ya asili.
0 maoni:
Chapisha Maoni