Pages

Jumatano, 21 Desemba 2016

DAR- CCM WAMPNGEZA RAIS MAGUFULI

 Image result for magufuli tanzania

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam kimempongeza Rais Dkt John Magufuli kwa uchapakazi na utekelezaji mzuri wa Ilani ya uchaguzi ya chama hicho, lakini pia kwa kuendesha vyema vikao vya kamati kuu ya chama hicho.

Pongezi hizo zilitolewa na Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba, alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

“Rais Magufuli ameendesha vikao kwa muda mfupi, lakini kwa mafanikio makubwa na sisi kama CCM mkoa tutahakikisha tunashirikiana kwa karibu zaidi na viongozi wa taifa walioteuliwa hivi karibuni,” alisema Simba.

Aliongeza kuwa pamoja na Rais Magufuli kuendesha vikao hivyo kwa muda mfupi, lakini ameweza kutoa maamuzi mazito yenye lengo la kukijenga chama hicho kwa siku moja

0 maoni:

Chapisha Maoni