Na Alex Mwenda
Duru la Pili la Ligi Kuu soka ya Wanawake ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF), linatarajiwa kuanza kesho Jumatano Januari 4, 2017
kwa michezo minne itakayofanyika kwenye viwanja mbalimbali.
Kwa mujibu wa ratiba, katika kundi ‘A’ pekee litakuwa na mchezo mmoja
wakati kundi ‘B’ litakuwa na michezo mitatu kwa siku ya kesho Jumatano.
Mchezo pekee wa kesho wa kundi ‘A’ utakuwa kati ya Mburahati Queens
ya Kinondoni, Dar es Salaam na Viva Queens ya Mtwara – mchezo
utakaofanyika Uwanja wa Karume jijini katika mzunguko wa sita wa ligi
hiyo.
Kabla ya michezo ya juma lijalo, upande wa Kundi A michezo yake miwili ya mzunguko wa sita itafanyika Alhamisi Januari 5, mwaka huu ambako Evergreen ya Temeke, Dar es Salaam itacheza na Fair Play ya Tanga kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Mlandizi ya Pwani inatarajiwa kuikaribisha JKT Queens ya Dar es Salaam, katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Mabatini.
0 maoni:
Chapisha Maoni